Tuesday, November 17, 2015
NINI HATIMA YA TAIFA LETU
KOBE 201 WALIOKUWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.
Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa
kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa
hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa
Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika
tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum
(sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao
walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia.

Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni
baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola.

RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo Ubalozini hapo.
………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.

Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November 17, 2015
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November 17, 2015
MAGARI MAZURI TOYOTA
ONLY 10 DAYS LEFT!! Wahi sasa kwa kujishindia TOYOTA IST!!
ZAWADI HII YA GARI IMESHAFIKA TANZANIA!!
Fuata maelezo ya jinsi ya kujiunga hapa:
http://www.beforward.jp/beforward_tanzania_campaign
...See MoreZAWADI HII YA GARI IMESHAFIKA TANZANIA!!
Fuata maelezo ya jinsi ya kujiunga hapa:
http://www.beforward.jp/beforward_tanzania_campaign
KAGAME MWENDO MDUNDO RWANDA
Bunge lamwezesha Kagame kuwania muhula wa 3 http://bbc.in/1l2njYu
Bunge la Senate la Rwanda limeidhinisha marekebisho katika katiba yatakayomuwezesha rais Paul Kagame kugombea urais kwa muhula wa tatu.
ALHAMDULILAH KWA STARS
Huwa nikiwaambia tz hamna timu ya ushindi mnatukana na kusema cyo mzalendo sasa leo ndo mtajua kama waarabu ni timu yenye vigezo vya kwenda world cup na cyo tz yenye maveteran watupu! mmeshindwa kura ktk sahani mkashiba huko kwenye bakuli ndo itakuaje!! miundo mbinu ya soka la bongo mibovu tu vipaji vpo havitazamwi tutaendelea kuwasindikiza mpaka mwisho!
dodoma kimenuka bunge la 11
WAKATI wabunge wateule wakianza kujisajili leo tayari kwa vikao muhimu vya kwanza vya Bunge la 11 wiki ijayo ikiwamo kumchagua Spika na Waziri Mkuu, Serikali ya Mkoa wa Dodoma imesema imejipanga vyema kuupokea ugeni huo na kuuhudumia huku ikisisitiza amri iliyowekwa ya kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano iko palepale.
Wabunge wametakiwa kujisajili kuanzia leo mjini hapa hadi keshokutwa Jumapili, wakati Jumatatu ijayo itakuwa ni siku ya kupeana maelekezo, kutembelea Ukumbi wa Bunge na mikutano ya kamati za vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ofisi ya Bunge iliyotolewa wiki iliyopita, Jumanne ya Novemba 17, itakuwa siku ya kuanza kwa kikao cha kwanza kwa kusomwa Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge, ikifuatiwa na uchaguzi wa Spika, Kiapo cha Uaminifu na Kiapo cha Spika na kisha Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote.
Wabunge wataendelea kuapa hadi Alhamisi asubuhi, na kisha jioni watathibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na kisha ataapishwa. Ijumaa, Rais John Magufuli atalihutubia Bunge.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kutokana na kuanza upya kwa pilikapilika za kisiasa hususani vikao vya Bunge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alisema amri hiyo ya kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa bado inaendelea ili kuweka utulivu muda wote wa vikao vya Bunge.
“Amri ya kuzuia mikutano wakati wa Bunge iliwekwa na Kamati nzima ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wetu ili kuwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake bila kubughudhiwa na watu au vikundi fulani vyenye nia mbaya ya kuvuruga usalama wetu,” alifafanua Galawa.
Wabunge na wageni mbalimbali wameshaanza kuwasili mjini Dodoma na Galawa aliweka wazi kuwa mkoa umejipanga vizuri kuwapokea na kuwahudumia wabunge na wageni wote watakaoingia. Alisema mkoa una uzoefu wa kuwapokea wageni wengi kwa mara moja kwa muda mrefu hivyo kila atakayekuja asiwe na wasiwasi wa mahali pa kufikia.
Kuhusu hali ya ulinzi na usalama wakati wa Bunge, mkuu huyo wa mkoa alisema wamejipanga vizuri na kuwaahidi kuwa wageni wote wataondoka salama, na kwamba yeyote atakayethubutu kuchezea hali hiyo ya usalama, atachukuliwa hatua kali za kisheria kwani hawatakuwa na mchezo katika hilo.
Aidha, aliwashauri wafanyabiashara wa nyanja zote mkoani kutumia fursa hiyo ya kuingia kwa wabunge hao na wageni wao kujiongezea kipato katika biashara zao. Aliongeza kuwa kama watawahudumia vizuri watajipatia wateja katika kipindi hiki na wengine kuwa nao kwa kipindi cha miaka mitano ya uhai wa Bunge la 11.
- Aliwataja wafanyabiashara wenye fursa hizo kuwa ni wenye hoteli, wauza vyakula, maduka, sokoni pamoja na wajasiriamali wadogo. Kuhusu makaribisho rasmi kwa Dk Magufuli alisema mkoa unaendelea kuwasiliana na Ikulu kujua ratiba kamili ya shughuli za Rais atakapokuwa mkoani katika ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani Novemba 5
Subscribe to:
Posts (Atom)