Saturday, December 5, 2015

Saturday, December 5, 2015

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam Awaagiza Wakurugenzi Kuwaondoa Ombaomba Waliko Barabara za Jiji


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.
 
“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.
 
Alisema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
 
Aidha, aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria
 
BOMU LA NYUKLIA NA HISTORIA YAKE FUPI.
Bomu la nyuklia hutengenezwa kutokana na madini yenye asili ya Radioactive kama vile Uraninum au Plutonium.  Madini haya yana tabia kuwa yakistuliwa kidogo tu basi yanaanza process inayoitwa nuclear fission ambapo hupasuka vipande vidogo vidogo huku yakiwa ...
Translate

KIM KARDASHIAN AND KANYE WELCOMES BABY NO.2

 
0 Comments
 Its a baby boy for this hollywood couple,and the baby came earlier than expected. You might have read it last week that the couple was struggling to settle on the NAME for their son,well...he is here!
 According to TMZ,family members have confirmed that both baby and mama are doing well.
Kim had posted this picture saying she is ready when..and it looks like the baby was ready as well..

magufuli nomah


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.

“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.

Alisema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.

Aidha, aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria

Tuesday, November 24, 2015

pm of tanzania

Waziri Mkuu Majaliwa aapishwa

maj1NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM
SIKU moja baada ya Kassim Majaliwa kuteuliwa na Rais John Magufuli na kuthibitishwa na Bunge kwa asilimia 73.5 kuwa Waziri Mkuu, jana aliapishwa kuanza kazi rasmi katika wadhifa huo.
Majaliwa, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, aliapishwa na Rais Magufuli majira ya asubuhi katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chamwino, mjini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakuu wa vyombo vya ulinzi pamoja na viongozi wastaafu.
Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na watu wa kada mbalimbali, wakiwemo viongozi na wanasiasa, pia lilihudhuriwa na familia ya Majaliwa, ikiongozwa na mke wake, Mary Majaliwa, watoto wake pamoja na ndugu wengine.
Majaliwa alikula kiapo chake cha uaminifu mbele ya Rais Magufuli akiwa ameshikilia Msahafu na kusoma mwongozo wa kiapo ambao uligawanyika katika sehemu tatu na kila alipomaliza sehemu moja alisema, “Ee Mwenyenzi Mungu nisaidie” na mara zote alikuwa akishangiliwa.
Alianza kusoma kipengele cha kwanza cha kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikafuatiwa na kipengele cha kufanya kazi bila upendeleo na kuzingatia sheria, akamalizia na kipengele cha kutunza siri ya Baraza la Mawaziri.
Baada ya kumaliza kula kiapo  lilifuatia tukio la viongozi kutoa mkono wa pongezi kwa Waziri Mkuu huyo mpya ambapo waliitwa kwa majina mmoja mmoja na kwenda kumshika mkono.
Rais Magufuli ndiye aliyeanza kumpa mkono wa pongezi akifuatiwa na Makamu wake, Samia Hassan Suluhu; Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa pili, Balozi Seif Ali Idi; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Pandu Amir Kificho, Spika wa Bunge la SMZ na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande.
Wengine waliompa mkono wa pongezi ni Jaji Mkuu wa SMZ, Omar Othman Makungu; Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue; Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Abdulhamid Yahya Mzee akafuatiwa na mke wa Majaliwa, Mary Majaliwa na baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano, George Masaju.
Makamu wa Rais mstaafu, Mohamed Gharib Bilal, aliliwakilisha kundi la viongozi wastaafu kutoa mkono wa pongezi kwa Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia viongozi hao wote pamoja na ndugu wa Waziri Mkuu walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na baadaye wakaendelea na shamrashamra zilizopambwa na ngoma kabla ya kuelekea bungeni kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge ya Rais Magufuli.

MAALIM SEIF, LOWASSA, SUMAYE WASUSA TENA
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameendelea kutohudhuria sherehe za kuapishwa viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya tano tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania bara na kufutwa kwa matokeo yote ya Uchaguzi wa Zanzibar.
Maalim Seif, ambaye hakuonekana jana wakati Majaliwa akiapishwa, hii ni mara ya pili kwake kutohudhuria sherehe kama hizo ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni wakati Rais John Magufuli akiapishwa Novemba 5, mwaka huu, baada ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza kususia sherehe hizo.
Msimamo huo wa Ukawa ulitokana na kile walichodai ni kutoridhishwa kwao na mchakato wa uchaguzi, hususan matokeo ya urais ambayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi, yakishatangazwa hakuna haki ya kuyapinga katika mahakama yoyote.
Viongozi wengine ambao nao walitakiwa kushiriki katika sherehe hizo na ambao hawakuhudhuria zote ni Mawaziri Wakuu wastaafu, Federick Sumaye na Edward Lowassa, ambao wote walikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia upinzani wakiiunga mkono Ukawa.
Sababu nyingine zilizotajwa za viongozi hao kutohudhuria matukio hayo makubwa ya kitaifa ni kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichodai ni kuwepo kwa kasoro nyingi katika uchaguzi huo.

Mtanzania
Read more

hapa kazi tu na magufuri

'Elimu bure' isizalishe wahitimu wasio na maarifa

24th November 2015
Chapa
Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli ameahidi kuanzia Januari, 2016 serikali ihakikishe inatoa  elimu bure kwa wanafunzi wote shule za msingi na sekondari za sekondari.
 
Watoto wanahudhuria shuleni, lakini swali kubwa la kujiuliza ‘je, wanajifunza?’. 
 
Taarifa za utafiti kadhaa, zimeonesha kuwa watoto wengi wanafika hadi Darasa la saba lakini hawana maarifa na Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK). Stadi hizi ni muhimu sana kwa ajili ya ngazi za juu za elimu au kupata maarifa mengine yoyote katika jamii.
 
Kwa mfano kulingana na malengo ya mtaala wa elimu ya msingi ya Tanzania, watoto wa darasa la tatu na kuendelea wanapaswa kuwa na Stadi za Ngazi ya Darasa la Pili za Kusoma na Kuhesabu. Hata hivyo, Tathmini za Uwezo za Miaka kadhaa (2011, 2012, 2014 na 2015) zimeonesha kuwa, watoto wengi wa darasa la tatu na kuendelea, wamekuwa na kiwango hafifu cha stadi za KKK. Zaidi sana kiwango duni sana kinajitokeza kwa somo la Kiingereza.
 
Iwapo watoto wetu wanakamilisha elimu ya msingi bila kuwa na stadi za msingi za KKK, ambazo ni muhimu sana kuwawezesha kumudu masomo ya ngazi za juu, tunapaswa kuwa na mashaka sana juu ya hatima ya watoto wetu. 
 
Mathalani tathmini ya Uwezo hapo awali, unajenga hoja yangu kuwa kupiga jaramba juu ya ‘elimu ya bure’ bila kuwa na mipango mahsusi na rasilimali za kutosha kuwekeza kwa umakini kunaweza kusababisha kuwa na kizazi cha wahitimu ambao hawana maarifa. 
 
Hii ikiwa na maana kuwa wamepitia elimu ya msingi, lakini mazingira katika shule zetu hayakuwawezesha kupata stadi na maarifa stahiki kwa ngazi husika ya elimu.
 
Mzazi umepata kujiuliza, ‘kwa nini mtoto wangu anaenda shule, lakini hakuna stadi wala maarifa anayojifunza?’
 
Kuna sababu kadhaa zinazosababisha watoto wetu wasipate stadi na maarifa tunayotarajia wapate huko shuleni. 
Baadhi ya sababu zinazopelekea watoto kupata stadi na maarifa hafifu:
 
Kwanza, mahudhurio hafifu au utoro:kuhudhuria shule ni moja ya sababu muhimu sana kumwezesha mtoto kujifunza vizuri. Mahudhurio hafifu au utoro wa muda mrefu husababisha matokeo hafifu ya kujifunza. Mfano, wakati wa Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2013, ilidhihirika kuwa kiwango cha mahudhurio kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule zilizofanyiwa Tathmini kilikuwa chini ya asilimia 40 kwa wanafunzi wa kike na wa kiume.
 
Tofauti ya mahudhurio shuleni kimkoa pia ilidhihirika. Mkoa wa Kilimanjaro ulionyesha mahudhurio ya juu kwa asilimia 81, wakati mkoa wa Kigoma ulikuwa na kiwango cha chini kwa asilimia 56. Ukifuatilia matokeo ya mitihani katika mikoa hii yanaendana sawia na kiwango cha mahudhurio.
 
Wataalmu wa elimu wanaafikiana kuwa, wanafunzi ambao hawana mahudhurio mazuri shukeni hukosa maarifa stahiki, na wengi huishia kuacha shule mapema na wanaweza kukosa ajira kwa muda mrefu, na kuingia katika lindi la umaskini.
 
Watendaji katika sekta ya elimu kwa ushirikiano na wadau wa elimu ikiwemo wazazi, wanaweza kukabiliana na changamoto hii ya utoro na mahudhurio hafifu ili kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni, na hatimaye wanafunzi kupata stadi na maarifa stahiki.
 
Mahudhurio au utoro wa walimu husababisha wanafunzi wakose muda wa kupata stadi na maarifa stahiki. Hii huathiri sana matokeo ya baadaye ya wanafunzi husika. Mfano matokeo ya Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2015, yalionesha kuwa, wastani wa taifa wa mahudhurio ya walimu ni asilimia 75. 
 
Kwa maneno mengine, Mwalimu mmoja kati ya walimu wanne hakuhudhuria shuleni siku ambayo Tathmini ya Uwezo ilifanywa. 
 
Takwimu nyingine zinaonesha kuwa, walimu watatu kati ya walimu 10 hawakuwepo shuleni katika mikoa ya Pwani na Mwanza; halikadhalika chini ya walimu wawili kati ya 10 hawakuwepo shuleni katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Kagera, wakati Tathmini ya Uwezo ilipokuwa ikifanyika.
 
Pili, uwiano kati ya idadi ya walimu na wanafunzi: kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, wanafunzi wengi sana wameandikishwa katika shule za msingi, wakati idadi ya walimu walioajiriwa ni wachache sana.
 
Hali hii imesababisha kuongezeka kwa mzigo wa kufundisha kwa walimu. Kuna shule ambazo Mwalimu anafundisha darasa la wanafunzi hadi 120! Hali hii huweza kusababisha Mwalimu akakosa muda wa kutoa msaada wa moja kwa moja kwa kila mwanafunzi anayehitaji msaada wa ziada katika kujifunza. 
 
Tatu, mazingira hafifu ya shule.Kukosekana kwa vitendea kazi na huduma muhimu shuleni kama vile madarasa, vitabu, vyoo, maktaba, na huduma kama vile maji salama ya kunywa, chakula na huduma za afya, ni mambo muhimu sana kwa mazingira ya shule. 
 
Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2015 inaonesha kuwa, shule nyingi zina huduma chache au hazina kabisa huduma hizi, hivyo kusababisha mazingira ya shule yasiwe rafiki kwa kujifunza. 
 
Nne, uwiano wa chumba cha darasa na wanafunzi: Sera ya Elimu inaelekeza kuwa, uwiano kati ya darasa na idadi ya wanfunzi ni chumba kimoja kitumiwe na wanafunzi 45 (1:45) kwa shule za msingi, wakati kwa shule za awali chumba kimoja kinatakiwa kitumike kwa wanafunzi 25. 
 
Hata hivyo, katika shule nyingi uwiano huu huwa mkubwa na watoto husongamana katika chumba cha darasa. Mfano, wakati wa Tathmini ya Uwezo ya 2015, katika Shule ya Msingi ya Mshikamano, ilionesha kuwa kuna watoto 126 wa shule ya awali, ambao wamesongamana katika madarasa mawili. 
 
Hapa ilitakiwa kuwe na vyumba vitano vya shule ya awali  kutosheleza mahitaji ya Sera ya Elimu, ili watoto wajifunze vizuri. 
 
Tutambue kuwa msongamano madarasani huathiri kujifunza kwa watoto wetu hasa wa madarasa ya awali.
 
Tano, baadhi ya walimu kukosa ari ya kufundisha: katika nchi hii. Walimu wamekuwa ‘mashujaa waliosahaulika’. 
 
Tumesahau kuwa wao tumewakabidhi jukumu la kuumba akili za watoto wetu ili kutimiza malengo ya Taifa katika kupata rasilimali watu ya kuwa viongozi, wataalamu na wananchi waliostaarabika kwa maendeleo ya Taifa letu. 
 
Sita, mafunzo kwa walimu. Walimu ambao hawapati mafunzo kazini mara kwa mara hupungukiwa maarifa. Kwa hoja hii, ile dhana ya ‘Elimu ya Msingi kwa Wote’ (kwa kiingereza ni Universal Primary Education (UPE), hii ‘UPE’ ilitafsiriwa kwa kejeli kama ‘Ualimu Pasipo Elimu’
 
Mipango na usimamizi mbovu wa sekta ya elimu: huenda tatizo kubwa isiwe ni udahili wa watoto wengi shuleni, lakini usimamizi mbovu wa sekta ya elimu kuanzia Wizara ya elimu hadi ngazi ya taasisi za elimu ndiyo shida kubwa sana, inayopelekea matokeo mabaya tunayoyaona sasa. 
 
Hivi shule ya msingi inawezaje ikaendeshwa kwa mafanikio iwapo ruzuku ya elimu inakawia kufika, na katika kiwango kidogo? Iweje kiwango cha elimu kikue wakati walimu wanalipwa mshahara mdogo, lakini zaidi hata huo mshahara mdogo hukawia sana kulipwa? 
 
Shule zitakuwaje na viwango vya juu, wakati wakaguzi hawajawahi kufika zaidi ya miaka mitano? Ni vipi viwango vya ufundishaji na ufaulu vifikiwe wakati shule hazina vifaa muhimu? Ni vipi viwango vya ufundishaji na ufaulu viboreshwe  wakatiwakuu wa shule wanateuliwa bila kuzingatia ujuzi na maarifa yao, na hawapati mafunzo ya uongozi?
 
Ni pale tu tutakapoweka juhudi katika kuimarisha mipango na usimamizi wa sekta ya elimu ndiyo tutaongeza viwango vya ubora wa elimu yetu.
 
Kwa kipindi kirefu tumeweka lengo katika kufaulu mitihani kuliko kuhakikisha watoto wetu wanapata ujuzi na maarifa. 
 
Hivyo, walimu huwalazimisha watoto wetu kusoma kwa kukariri ili wafaulu mitihani, na hawafundishwi kuwa na uwezo wa kutafakari na kuhoji mambo. Kwa sasa mwanafunzi anayepata ‘A’ au Daraja la kwanza, haimaniishi ni mwenye ujuzi wala maarifa, hutegemea kama alichokariri tu kilitokea katika mtihani. Kuna wakati nadhani mitihani haiwezi kupima kiwango cha maarifa ya mtu.
 
Kukosekana kwa rasilimali za kutosha: kiasi kikubwa cha bajeti yetu hutegemea wafadhili wa nje. Hivyo, wakitetereka tu kidogo katika kutoa msaada basi na programu zetu za elimu nazo zinatetereka. Kuna umuhimu kukuza vyanzo vya ndani vya mapato ili kusaidia elimu yetu. 
 
Ili kuweka mambo sawa tunahitaji kuchambua elimu yetu ya sasa, kuwe na utashi na dhamira ya dhati ya kisiasa, mipango bora, uwekezaji wa uhakika, mafunzo bora ya walimu, kuhuishwa mitaala na mfumo bora wa udhibiti wa ubora

Thursday, November 19, 2015

masomo ya afya nini chanzo na matibabu yak

Kuna magonjwa mengi tofauti ya akili yanayoathiri ubongo wa binadamu na magonjwa haya ni kama yale yajulikanayo kwa majina ya bipolar disorder,huzuni ya kupindukia, schizophrenia, hali ya wasiwasi na  yamagonjwa ya  akili disordersyanayoathiri vile ambavyo mtu huwaza na huhisi.
 Chanzo kamili cha  hakijulikani lakini kinachojulikana ni kwamba haya magonjwa hayatokani na kasoro ya kitabia au kasoro yoyote ya kiutu.
 Kutokana na tafiti mbalimbali, haya ni magonjwa kama magonjwa mengine kwasababu kadha wa kadha zinazodhaniwa ndizo sababishi za magonjwa hayo.
Baadhi ya sababu hizo ni mabadiliko katika umbo la bongo ambapo mabadiliko hayo huathiri  ubongo, hisia na tabia za mtu, mazingira ya mtu, uhusiano wake na watu wengine, maisha ya jamii na masaibu ya maisha kwa wakati mwingine huchangia magonjwa ya kichaa.
 Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, jamii tuishiyo, wanaume na wanawake wana nafasi sawa ya kuathiriwa maishani ingawaje wanaume ndio mara nyingi huathiriwa mapema maishani mwao.
 Tafiti zinaonyesha kuwa kuna aina mbili ya magonjwa ya akili na dalili za haya magonjwa zimetofautiana, mfano Psychosis, hii hutokea pale Mtu hushikwa na hali ya wendawazimu na kuchanganyikiwa, Mood disorders hutokea pale mtu hushikwa na huzuni ya kupindukia, wasiwasi, woga, ukosefu wa usingizi, ukosefu wa hamu na mambo ambayo mtu hupenda kufanya na ukosefu wa hamu ya kula hivyo mabadiliko haya ambayo yanaweza kutokea ghafla au pole pole hufanya iwe vigumu kusoma, kufanya kazi au kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wengine.
 Karibia magonjwa yote ya akili yanatibika au madhara yake kupunguzwa kupitia matibabu,psychotherapy au mashauri lakini Uponyaji wa haya magonjwa hurahisishwa wakati watu wanapoelewa na kuwatunza kwa njia ya kiutu wale ambao wameathiriwa.
 Katika jamii mbalimbali, mtu aliyeathiriwa mara nyingi hubaguliwa na kutengwa na watu wengine kwasababu ya hali aliyonayo au wakati mwingine kutoelewa tabia ya mtu mwenye ugonjwa huo.
 Ni jambo la muhimu kuzingatia tabia za mila ya aliyeathiriwa wakati anapotibiwa ili aweze kupona na hatunabudi kuonyesha upendo na uelewano ambao utamsaidia mgonjwa huyo kurejea katika hali yake ya kawaida kama wengine.
 Tafiti zinaonyesha kuwa ugonjwa wa akili huathiri mara nyingi watu wa umri kuanzia miaka 15 hadi 25 kwa mara ya kwanza, ingawaje ugonjwa huo unaweza kutokea baadaye maishani.
 Theluthi moja ya walioathiriwa na ugonjwa wa akili hukumbwa na kipindi kimoja ama vichache vifupi tu maishani ingawa kwa wengine huendelea kuathiriwa kwa kurudiarudia maishani mwao ambapo mwanzo wa ugonjwa huu unaweza kutokea ghafla na dalili kali kuonekana zaidi wiki zinazofuata au unaweza kuathiri mtu polepole, na kuonekana kwa miezi au hata miaka.
 Hapo mwanzoni, aliyeathiriwa hujitenga na watu, huwa na huzuni na hali ya wasi wasi, yeye pia huwa na mawazo ya kustaajabisha au hofu nyingi hivyo kuna haja na umuhimu wa kufahamu dalili kwa mtu huyo ili aweze kupata matibabu mapema.
 Utambuzi mapema wa dalili hizo na kuchukua hatua zifaazo kutibu kwa mgonjwa wa akili ni muhimu kwani kutoelewa ugonjwa huu kunasababisha unyanyapaa, upweke na ubaguzi unaoweza kuathiri wale walio patwa na ugonjwa wa akili na jamii zao pia zinazowatunza.
 Bwana Thaddeus Kamisa ni mwanafunzi aliyehitimu Shahada ya mambo ya Jamii (Sociology) katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kilichopo jijini Mwanza ambaye pia amewahi kufanya kazi katika baadhi ya Mashirika yanayojihusisha na watu wenye Ugonjwa wa Akili kama vile Basic Needs anabainisha dalili mbalimbali kuu za magonjwa ya akili.
 Bwana Kamisa alisema kuwa, baadhi ya dalili za ugonjwa wa akili ni pale mtu kuwa na Maono ya uwongo ama imani ya uwongo ya kudhulumiwa, kujilaumu au mambo makubwa au kutawaliwa na mwengine inaweza kupelekea kupatwa na ugonjwa huo. Mtu huyo hufikiri kwamba watu fulani wanapanga njama dhidi yake ama ana nguvu zisizo za kawaida na wakati mwingine waathiriwa watajitenga na kujificha ili kukwepa hizo dhuluma anazoziwaza.
Anaeleza kuwa, mtu kupotewa akili ni dalili nyingine ambapo kwa kawaida inahusisha kusikia sauti inayotokea lakini sio sana ikiwemo kuona, kugusa, kuonja au kunusa mambo mengine anayodhani ni ya kweli ingawa havipo.
 Pia mawazo ya fujo yanachangia hasa hutokea pale mtu huyo pindi anapopatwa na ugonjwa kama huo kuongea kwake huathirika mpaka ni vigumu kufahamu maongezi yake muda mwingine anakuwa anatamka maneno kwa njia isiyoeleweka na isiyo na maana.
“Dalili nyingine za ugonjwa wa akili hutokea pale mtu anapokosa hamu ya kutenda mambo ya kawaida ya kila siku, kama kufua au kupika na kupoteza uwezo kufanya hivyo, kukosa hamu ya kutenda, uhamisisha na moyo wa kujituma siyo uvivu bali ni vile ambavyo ugonjwa umemuathiri”, alisema Kamisa.
 Kamisa anaendelea kusema kuwa, wakati mwingine matatizo ya kufikiria uwezo wa mtu kuwa na kina, kukumbuka, kupanga na kutunga pia huathirika, hivyo inakuwa ni vigumu zaidi kufikiri, kuwasiliana na kufanya shughuli za kawaida.
 Akizungumzia kuhusu baadhi ya magonjwa ya akili ambayo yanaweza kuwaathiri baadhi ya vijana wa Tanzania, alisema kuwa, matumizi ya pombe na madawa ya kulevya, haswa bangi na madawa mengine yajulikanayo kama ‘amphetamine’ yanaweza kusababisha mtindio wa ubongo kwa vijana hao pia kwa watu ambao wanaweza kuathiriwa na mpumbao wa ubongo kiurahisi ingawaje matumizi ya madawa hausababishi mpumbao wa ubongo una uhusiano mkubwa na kipindi cha kuathiriwa kurudi.
 “Kwa mujibu wa takwimu za Kitaifa inasadidika kuwa  asilimia 61% ya  wagonjwa wa akili katika wilaya ya Ukererewe mkoani Mwanza ni vijana hali ambayo inachangia ongezeko la umasikini katika jamii”, alisema Kamisa.
Aliendelea kusema kuwa, tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa asilimia 20 ya vijana wote duniani wana tatizo la afya ya akili ambapo asilimia 85 ya vijana hao wanaishi katika nchi masikini ikiwemo Tanzania.
Kamisa alifafanua kuwa, kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, Tanzania inakadiliwa kuwa na watu wapatao  milioni 45  na kati yao vijana ni zaidi ya asilimia 35.
Aidha alibainisha kuwa, Sera ya maendeleo ya Taifa ya Vijana inasema kuwa kijana ni mtu mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 ikitofautiana na ile ya Umoja wa Mataifa  ambayo inayoonyesha kuwa ni mtu  kuanzia miaka 18 hadi 24. 
Ugonjwa wa akili kwa namna moja au nyingine umekuwa ukilikumba zaidi kundi la vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa huku ikidaiwa kuwa matumzi ya dawa za kulevya yana mchango mkubwa katika hilo.
Ili Taifa changa kama Tanzania liweze kupiga hatua za haraka za maendeleo  kwa vijana, Serikali pamoja na wadau wa maendeleo na jamii hawanabudi kuungana kwa pamoja katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu kazi ya taifa  hata kuwa kundi hatarishi katika jamii kwa sababu ya kufanya matukio ya kuhatarisha maisha. 
Tanzania ni miongoni mwa nchi  zilizoridhia Mikataba mbalimbali kuhusu afya ya akili licha ya tatizo hili kutokabiliwa kikamilifu kutokana sababu mbambali zikiwemo za umasikini na ukweli kuwa wagonjwa wanaendelea kuongezeka licha ya kuwa hakuna takwimu sahihi.
Takwimu za Kanisa Katoliki nchini Tanzania zinaonyesha zaidi ya wagonjwa wa akili 68,000 wamepatiwa huduma za afya katika kituo cha Shirika la Mitume la Brothers of Charity kilichopo Marumba mkoani Kigoma kati yao wagonjwa 25,000 walilazwa na kuruhusiwa kuondoka baada ya kupata nafuu na Wagonjwa wa akili 43,000 walipata huduma kwa nyakati tofauti wakitokea majumbani mwao baada ya kupewa maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa.
Uchunguzi wa afya ya akili duniani uliofanyika mwaka 1990 ulibaini kuwa, maradhi hayo yalichangia asilimia 10.5 ya usumbufu na ufanisi duni ikilinganishwa na magonjwa mengine katika jamii na kwamba ifikapo mwaka 2020 magonjwa hayo yatachangia aslimia 15 ya usumbufu na ufanisi duni katika kukabiliana na maisha. 
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya magonjwa 10 yanayoongoza kusababisha hali ya ulemavu duniani, matano kati ya hayo ni magonjwa ya akili yanayochangia  asilimia 28 ya maisha duni katika jamii.
Pia inaelezwa kuwa, ugonjwa wa Sonona (‘Depression’) ni hatari sana katika jamii na kwamba ni ugonjwa mtambuka kwa sababu baadhi ya watu huupata kutokana na kuwa na vina saba vya ugonjwa huo, dawa za kulevya na misongo ya mawazo.
Hali halisi ni kwamba  limekuwa jambo la kawaida sana kuwaona baadhi ya wagonjwa wa akili wakiokota makopo,vyakula jalalani na wengine kushinda wakizurura mchana kutwa mitaani pasipo kutambua hatma ya maisha yao, hivyo jamii inapaswa kuwasaidia watu wa aina hii kwa kuwapatia misaada ya malazi na chakula. 
Daima jamii ikumbuke kwamba, siyo tu kuwa watu wote wenye matatizo ya akili walitumia dawa ya kulevya bali kuna waliozaliwa wakiwa na tatizo hilo, na wengine ilitokana na msongo wa mawazo, kutokana na hali hiyo ni vema tukatambua kuwa kila aliye na akili timamu leo anaweza kuwa mgojwa wa akili kesho.
Kwa ujumla wananchi na viongozi wa kijamii wote kuna umuhimu mkubwa wa kulisemea kundi hilo kutokana na matatizo makubwa yanayowakumba,  badala ya kufikiria manufaa yetu na kuwaacha  wakiwa gizani wasijue la kufanya katika jamii. 
Ifahamike pia watu hawa wana haki zao zinazolindwa kama watu wengine  kwani kuna umuhimu wa kuwathamini na kuwapatia mahitaji yao yote ya msingi badala ya kuendelea kuwaona kama mizigo katika familia na jamii, hivyo wanastahili matibabu, chakula na mahitaji yao mengine muhimu.

tingatinga la pita dar

zilizotufikia

jamani

Hii ni ya kichanga aliyezaliwa na kukutwa na ujauzito wa mapacha !!

on
twins-1Mara nyingi tumezoea kusikia matukio ya ajabu, mengine yakiingia kwenye historia na kuacha kumbukumbu zisizofutika kama hii ya mtoto aliyezaliwa China na kugundulika kuwa ni mjamzito.
Mtoto huyo aliyezaliwa Katika Hospitali ya Queen Elizabeth na kugundulika kuwa ana ujauzito wa watoto mapacha wiki tatu tangu azaliwe kitendo kilichowalazimu madaktari kumfanyiwa upasuaji.
Daktari bingwa wa uzazi Dr Yu Kai-man amesema haikuwa rahisi kumchunguza mtoto huyo ili kujua ujauzito huo, kwa kuwa ujauzito huo ulikuwa mdogo sana na haikuwa rahisi kufikiri kwamba mtoto huyo mdogo anaweza kupata ujauzito.
Taarifa zinasema tukio kama hili lilitokea mwaka 2010 ambapo lilimtokea msichana ambaye hajafahamika, Shirika la Afya Duniani lilisema hiyo inaweza kuwa aina ya  cancer na inaweza kuhusishwa na kitendo cha mama kutoa sana ujauzito.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitterInsta Facebook