Thursday, November 12, 2015

ZIRA YA KUSHITUKIZA YA RAISI MAGUFULI KATIKA HOSIPITARI YA MHIMBILI

Rais wa Tanzania Dk.John Maguli amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya taifa muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Attached Thumbnails Attached ThumbnailsClick image for larger version. 

Name: 111.JPG 
Views: 25989 
Size: 80.4 KB 
ID: 304829   Click image for larger version. 

Name: 222.JPG 
Views: 26880 
Size: 125.8 KB 
ID: 304830   Click image for larger version. 

Name: 333.JPG 
Views: 26005 
Size: 69.9 KB 
ID: 304831   Click image for larger version. 

Name: IMG-20151109-WA0028.jpg 
Views: 25455 
Size: 119.0 KB 
ID: 304832   Click image for larger version. 

Name: IMG-20151109-WA0026.jpg 
Views: 25458 
Size: 146.6 KB 
ID: 304833  

NJOMBE

MAKALA.
NINI SULUHISHO LA TATIZO LA MAJI NJOMBE?
Na jimsoni myinga;

         Maji ni kimiminika mhimu sana kwa maisha ya kila siku kwa binadamu yeyote, maji yana umuhimu mkubwa sana katika kuletea maendeleo ya eneo lolote lile, maji pia ni muhimu sana katika maisha ya viumbe hai kama mimea,wadudu na wanyama.
Vipo vyanzo vingi sana vya maji kuna mabwawa,mito na maziwa.Kwa kuanza tatizo la maji njombe limekuwa kubwa sana kadri siku zinavyozidi kwenda, tatizo hilo la maji mkoa wa njombe limekuwa kubwa kiasi cha kufikia kukithiri sana baina ya wananchi na wakazi wa mkoa huu.                                                               
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoani njombe wakazi wa kata ya njombe mjini na kata ya ramadhani wamesena tatizo hilo la maji limekuwa kero sana kwao, wakiendelea kuelezea adha hiyo ya maji inyo wa kabili wananchi hao na wakazi wa mkoa huo wa njombe wamesema wanaomba mamlaka zote zinazo husika na kutatua tatizo hilo kulishughulikia tatizo hilo kwa haraka kadri inavyo wezekana.                            
Wakazi hao wa kata hizo za njombe mjini na ramadhani waliendelea kwakusema kuwa wamechoshwa na maneno na ahadi za wanasiasa na viongozi wengi waoishia kuwa ahidi tu kuwa watamaliza tatizo hilo haraka iwezekanvyo na hatimye hawa tekelezi  ahadi hizo kwa wakati.Wakiendelea kulalama kwa hisia wananchi hao mithiri ya mbogo walio jeruhiwa walisema tatizo hilo la maji limepelekea matatizo mengi sana kama vile watoto kuchelewa shule, hapa inasababishwa na foleni kubwa wanayo kumbana nayo pale wanapo jihimu kwajili ya kwenda kuyasaka maji hayo katika mabomba ambayo miundombinu yake imechoka sana nakuto mudu uhitaji wa wananchi wa maeneo hayo “yaani ni kama mgonjwa anakaribia kupoteza uhai wake”.
                    
Nilifurahishwa sana na kauli mbalimbali walizokuwa wakizitoa wakiziirisha dhahiri wamechoshwa na hali hiyo ya maisha wanayoishi na nukuu “wananchi tunapata shida mithiri ya wakimbizi katika nchi yetu wenyewe, tunataabika sana na wengine ndoa zetu zimekuwa hatarini kwasababui tu waumezetu wanakosa maji ya kuoga”.
Wakiendelea kutoa kero hizo wanasema pia maji ni muhimu sana katika kuimarisha afya zao, maji yanavyo kosekana wanashindwa kufanya usafi wa vyombo vyao na maeneo muhimu kama vyooni na mabafuni hali hiyo inapelekea kulipuka kwa magonjwa kama kipindupindu na homa za matumbo.
Ndipo nikalazimika kubisha hodi katika ofisi za mamlaka husika inayohusika na  “maji safi na maji taka” mkoani hapa.Nikizungumza na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani njombe amesema “Kama mamlaka tuna tambua uwepo wa tatizo la maji mkoani hapa na hali hii imesababishwa na ongezeko kubwa la watu mkoani hapa,Nasababu nyingne ikiwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya maji mkoani hapa”.
 Akizungumza mkurugenzi mtendaji huyo wa maji taka na maji safi  amesema tatizo hili lipo mbioni kutatuliwa kwakuwa kuna mradi mkubwa wa maji ambao mda sio mrefu utakuwa tayari na wananchi watapata maji yakutosha masaa24 na kusahau adha hiyo iliyo wakumba kwa mda mrefu.

Usikose kupata mwendelezo wa nakala hii wiki lijalo...................... 

ALIKIBA AZUNGUMZIA UWEZEKANO WA YEYE KUFANYA COLLABLE NA NGULI WA BONGO FLAVA NASIBU ABDULI DIAMOND


Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia.

Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko.

“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho kitu kipo.

 "Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! 

"Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” alisema AliKiba.


Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”

SIMULIZI ZENYE HISIA


SIMULIZI ZA KUSISIMUA

 SIMULIZI YA KOSA LANGU:
AUTHOR : ADELA DALLY KAVISHE
Joyce ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Ndesanjo, maisha yao yalikuwa ni maisha ya furaha na amani walikuwa wakiishi Mkoa wa Dar es salaam maeneo ya Kimara Stop Over, lakini furaha hiyo ilipotea baada ya siku moja ambapo Mzee Ndesanjo alikuja nyumbani baada ya kutoka kazini na moja kwa moja akimtaka mama Joyce ajiandae kwani wangesafiri siku hiyo ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni.Mzee Ndesanjo alikuwa na gari aina Eskudo alifika na kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama Joyce" huko chumbani mama Joyce alimskia na kuitika "Bee Mume wangu,vipi mbona unaonge kwa sauti sana si ungeingia ndani kwanza" alisema mamaJocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa makini Baba Joyce alimsogelea huku akisema "hakuna muda wa kupoteza mimi ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro kuna matatizo kwani rafiki yangu tunayefanya naye kazi  amefiwa na mke wake wake inabidi tuwahi kwenda"

mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari na kusema "mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa masikini" aliongea kwa masikitiko Baba Joyce akamjibu na kusema "alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke"  mama Joyce akasema "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani" aliuliza mama Joyce kwani kwa wakati huo Jocye na mdogo wake aliyeitwa James walikuwa wameenda shule Joyce alikuwa darasa la tano na James akiwa darasa la kwanza na pale walipokuwa wakiishi likuwa ni nyumba ya kupanga.Baba Joyce alimgeukia tena mke wake na kusema "hawa watoto tutamkabidhi jirani yetu Mzee Ngonyani na mkewe kwani hatuendi kukaa zaidi ya siku mbili wewe jiandae tuondoke wakirudi kutoka shule watakuta maagizo kutoka kwa mke wa Ngonyani" alisema baba Joyce.

Ndipo mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa kipindi cha siku mbili baada ya hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari ambapo safari ilianza wakiwa njiani maeneo ya  Kidatu ghafla gari lilipata pancha tairi ya mbele na kupinduka ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani Baba Joyce alifariki palepale na Mama Jocye alikuwa ameumia sana sehemu za kichwani hivyo wasamaria wema walimchukua na kumkimbisa hospitali,,,,nini kilitokea itaendelea

KOSA LANGU SEHEMU YA PILI

Baada ya wasamaria kumkimbiza hospitalini Mama Joyce ambaye kwa wakati huo alikuwa hajitambui  Askari  Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu wa Baba Joyce na kuupeleka chumba cha maiti hospitali ya Morogoro, gari lilikuwa limeharibika sana kutokana na ajali ilivyokuwa mbaya hivyo ulifanyka utaratibu wa kulisogeza hadi kituo cha polisi, wakiwa hospitalini Mama Joyce alikuwa hajitambui kabisa na hivyo Polisi waliamua kufanya utaratibu wa kufahamu ndugu ambao wangeweza kuwa naye karibu kwa wakati huo, mmoja wa mapolisi alimwambia mwenzake "sasa tutafanyaje kuwapata ndugu wa hawa watu kwani huyu mama hajitambui na mume wake amekwisha fariki inabidi tuwatafute ili waendelee na taratibu nyingine" mwenzake ambaye alikuwa naye akamjibu na kusema  "inabidi tupekue namba za simu katika simu zao na kuweza kuwasilia na ndugu zao" basi moja kwa moja alichukua simu ambayo ilikuwa ni ya baba Joyce na kuangalia namba za watu mbalimbali akiwa anatizama nani wa kumpigiia simu alijaribu jina ambalo lilikuwa kwenye simu ambalo liliandikwa Mkurugenzi alipiga namba hiyo bila mafanikio na alijaribu namba kama tatu zote zilikuwa hazipatikani.

Ndipo wakaamua kuchukua simu ya mama Joyce na kuangalia namba nyingine katika simu hiyo kwa bahati nzuri walikuta namba ya Mke wa Ngonyani ambayo ilikuwa imeandikwa Mama ngonyani na kujaribu kuipiga simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa hadi ikakata lakini waliendelea kujaribu hatimaye simu ilipokelewa,Mama Ngonyani ambaye ni jirani wa Mama Joyce aliyekuwa amekabidhiwa watoto alipokea ile simu akijua mke wa Ndesanjo ndiye aliyempigia na kusema "Habari mama joyce nilikuwa mbali na simu vipi mmekwishafika" yule askari aliyekuwa anasikiliza ile simu alinyamaza kimya kidogo na kusema "samahani mama unazungumza na askari polisi kutoka Morogoro" kabla hajaendelea Mama Ngonyani alimkatisha na kusema kwa mshangao "askari! kwani kuna nini tena mama Joyce yuko wapi?" aliuliza mama Ngonyani yule askari akamwambia usijali mama nilikuwa nataka kufahamu unamfahamu vipi Mama Joyce" kwa haraka Mama Ngonyani akajibu "Mama Joyce ni jirani yangu na pia ni rafiki yangu na wameenda Morogoro kwenye msiba sasa nashangaa kuzungumza na askari kupitia simu yake kwani kuna tatizo" alizungumza mama Ngonyani huku akitaka kufahamu nini kinaendelea ndipo yule askari akamwambia kile kilichotokea "Mama Joyce na mume wake wamepata ajali  maeneo ya kidatu na hapa ninapozungumza nipo hospitali ya Morogoro nilikuwa naomba ungewajulisha ndugu zake ili waje haraka" alizungumza yule askari lakini hakumwambia kama baba Joyce alikuwa amefariki.

kwa mshtuko mama Ngonyani akasema "Ajali? Mungu wangu jamani, kwahiyo wanaendeleaje sasa ndugu zake akinanani mimi ninachojua hawana ndugu zaidi ya watoto wao wawili Joyce na James ambao wapo hapa nyumbani na ni watoto wadogo sijui nifanyeje jamani" alizungumza maneno mengi kana kwamba mtu aliyechanganyikiwa kumbe masikini Mzee Ndesanjo na mke wake walikuwa hawana ndugu zaidi ya watoto wao yule askari alimsisitiza mama Joyce afike hospitali kwani kulikuwa hakuna mtu wa kumuhudumia mama Joyce basi Mama Ngonyani alimjulisha mumewe na haraka walijiandaa kwa safari ya Morogoro huku wakiwaacha Joyce na James bila kuwajulisha kile kilichotokea walipofika haospitalini ndipo walipogundua kuwa Baba Joyce alikuwa amefariki na hali ya mama Joyce ilikuwa mbaya sana walionana na daktari ambaye aliwaeleza iwapo mama Joyce akizinduka kuna uwezekano asikumbuke chochote kilichotokea kwani alikuwa ameumia sana maeneo ya kichwani maneno hayo yaliwasikitisha sana Mama Ngonyani na mume wake ambao waliamua kufanya utaratibu wa mazishi wakati huo Mama Joyce akiwa hajitambui walimuhamishia hospitali ya Muhimbili Dar es salaam  kuendelea na matibabu na huko nyumbani mazishi yalifanyika vilio na simanzi vilitawala watoto walilia sana kwa uchungu wakati huo na hata kupoteza fahamu huku wakiwa hawajui ni hatma ya mama yao mzazi hapo ndipo maisha ya Joyce na mdogo wake  yalianza kubadilika nini kitaendelea usikose sehemu ya tatu............

SIMULIZI YA KOSA LANGU SEHEMU YA TATU

Baada ya kumuhifadhi Marehemu kwenye makazi yake ya milele, watu walitawanyika pale nyumbani na kuwaacha akina Joyce wakiwa na simanzi na wakati huo waliishi kwa kumtegemea Mzee Ngonyani na mke wake,maisha yaliendelea huku baadhi ya watu wakitoa michango yao kwa ajili ya matibabu ya Mama Joyce ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Yule rafiki yake na marehemu mzee Ndesanjo alirudi Dar es salaam baada ya mazishi ya mke wake kule Morogoro na muda wote alikuwa hajui nini kimempata rafiki yake kipenzi kwani hata marafiki zake walimficha kwasababu naye pia alikuwa katika matatizo ya kufiwa na mke wake, aliporudi Dar es salaam alielekea nyumbani kwa marehemu ili kumjulia hali alipofika alimkuta Mama Ngonyani akiwa pamoja na Joyce wakiwa wanajiandaa kwenda hospitali kumuona mgonjwa Joyce alikuwa akimfahamu rafiki wa baba yake ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Beni basi alipomuona akaanza kumfuata huku akilia kwa uchungu “Baba mdogo Baba mdogo, ulikuwa wapi Baba yangu amefariki na mama anaumwa sana” Mzee Beni alimuangalia Joyce kwa makini kisha akasema “etii!Mzee Ndesanjo amefariki haiwezekani jamani nini kilitokea,siamini mimi haya maneno” alizungumza huku akiwa amemshika mkono Joyce aliyekuwa analia kwa uchungu.



Mama Ngonyani akamsimulia kila kitu kuhusu ajali waliyoipata marehemu Mzee Ndesanjo na mkewe wakati wakielekea msibani Morogoro, Mzee Ben aliinama kwa uchungu na kuanza kulia kwa kumpoteza rafiki yake,Baadaye waliondoka pamoja hadi hospitalini kwenda kumtizama Mama Joyce anaendelaje walipofika walimkuta amezinduka lakini alikuwa haongei chochote muda wote  alikuwa kimya na alimshangaa kila aliyekuwa anamuona Joyce aliyekuwa karibu na mama yake alimuita “mama, mama mimi mwanao Joyce ongea basi mama hata kidogo” alimuita bila mafanikio mama yake alibaki akimshangaa bila kusema chochote hali ile iliwatatiza sana Mzee Beni na Mama Ngonyani waliokuwa pale hospitalini iliwabidi waende kumuona Daktari ili waweze kufahamu zaidi, ndipo Daktari akawaeleza kuwa mgonjwa amepoteza kumbukumbu zote kwani katika hali aliyonayo hawezi kumkumbuka hata mtoto wake na pia kuna uwezekano hata kama akirudi katika hali yake basi atakuwa hana akili vizuri Mama Ngonyani kusikia hivyo alishtuka na kusema “Mungu wangu sasa itakuwaje ndiyo tumekwisha mpoteza mama Joyce, ina maana Daktari hakuna njia yoyote ya kumrudisha katika hali yake ya kawaida, tusaidie jamani” alizungumza mama Ngonyani huku machozi yakiwa yanamdondoka Daktari alimjibu akisema “Huwezekano hakuna kilichobaki ni Kumuomba Mungu amsaidie pia tunaweza kumruhusu kesho ili muweze kumuhudumia akiwa nyumbani”.



walibaki wanasikitika na kutafakari,  baadaye ilibidi waondoke na kesho yake walirudi kwaajili ya kumchukua mama Joyce ambaye alikuwa haelewi chochote.Maisha yalianza kubadilika kwa mtoto Joyce aliyekuwa na Malengo ya kusoma na baadaye kuwa Mwanasheria hali ilizidi kuwa ngumu kwani Mama Joyce alikuwa akihitaji huduma wakati wote ilifikia kipindi familia ya Mzee Ngonyani ikaanza kuwatenga na hata waliokuwa  marafiki waliwaacha wakitaabika wenyewe, Kutokana na hali kuwa mbaya  Joyce aliamua  kuacha masomo akiwa darasa la sita ili aweze kumsaidia mama yake pale nyumbani Mzee Ngonyani na Mkewe waliamua kuhama katika ile nyumba na tokea walipohama hawakuwahi kurudi hata siku moja kwenda kumsalimia mama Joyce, hali ilizidi kuwa mbaya Joyce na mdogo wake ilibidi wakati mwingine waende mitaani na kuomba msaada angalau wapate pesa ya kula pale nyumbani.



Siku moja Mama Joyce aliamka asubuhi kichwa kilikuwa kinamuuma sana hivyo alitakiwa apelekwe hospitali ambapo Joyce alikuwa hana chochote kwani alikuwa akitegemea biashara ya kuuza maandazi na pesa ilikuwa ni ndogo alihangaika sana bila kupata msaada wowote hatimaye Mama Joyce alifariki Dunia kutokana na kuumwa sana bila kupata matibabu, Aliwaacha  Joyce na James ambao sasa walikuwa ni yatima maisha yalikuwa magumu  hawakujua nini cha kufanya kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi walifukuzwa kutokana na kushindwa kulipa kodi, hivyo kujikuta wakirandaranda mitaani kutafuta kipato…… nini kitatokea huko mitaani na nini hatma yao usikose sehemu ya 4

MJUE MCHUNGAJI MTIKILA

SOMA HAPA SAFARI NZIMA YA MAISHA YA MAREHEMU MCH.MTIKILA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  MCHUNGAJI Christopher Mtikila ni Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) ambacho kina usajili wa kudumu hapa nchini.  Mtikila alizaliwa mwaka 1950 mkoani Iringa, kusini mwa nchi yetu. (Kwa bahati mbaya, hadi nachapisha uchambuzi huu sikupata taarifa za elimu yake) kwani hakuwa mwepesi kutoa ushirikiano mwezi mmoja uliopita alisafiri kwenda nje ya nchi na kurejea wakati nikiwa katika hatua za mwisho za uhariri. Pamoja na shughuli za siasa, Mchungaji Mtikila ni mwanzilishi...
You might also like:

HI NI KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

NINI KIMETOKEA JIMBO LA ISIMANI MKOANI IRINGA KWENYE UCHAGUZI ULIOPITA

Williamu lukuvi amembeza mpinzani wake katika jimbo la ismani‏


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi  Na fredy mgunda,Ismani MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo. Kauli ya Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji...
You might also like:

WHY ZARI THE BIG BOSS

Why Zari Won't Show Her Daughter's Face

Zari's baby, @princess_latiffah is less than 10 days old but the socialite is not about to show her daughter's face. The fans want to know whose features the celebrity baby with close to 90,000 followers on Instagram has taken. However, Zari and Tanzania's Diamond Platnumz are still weighing the options before the fans can eventually see the beautiful princess. What is causing the delay? Media...
Read more ... QUOTE: Love is friendship that has caught fire. It is quiet understanding, mutual confidence, sharing and forgiving. It is loyalty through good and bad times. It settles for less than perfection and makes allowances for human weaknesses

PATA STORY KARI ZA KIMAPENZI

Nimefanya Mapenzi na Shemeji yangu kwa Bahati Mbaya

I had séx with my brother-in-law by mistake. In the dark I thought he was my husband. I’m 29, my husband’s 31. His parents held a family party for his niece’s 18th birthday last weekend. Everyone was there, including my husband’s brother who was home from working away in Saudi. He’s 36. We all get on well and there was plenty of alcohol and food. It was a nice party and we carried on drinking...
Read more ... QUOTE: Love is friendship that has caught fire. It is quiet understanding, mutual confidence, sharing and forgiving. It is loyalty through good and bad times. It settles for less than perfection and makes allowances for human weaknesses.

MHE.JAKAYA MRISHO KIKWETE WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA RISI DK.JOHN POMBE MAGUFULI

sikiliza wimbo mtam wa mapenzi jaman ama kweli ni raha kwa wale wapendanao kwa dhati>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>.

                 
cheki mambo ya ki nigeria hayo apana chezea wewe>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

ECKROSS COLLEGE
PHOTOJOURNARISM

ASSIGMENT

Jimson myinga;

1: straight angle
2:high angle
3:side angle
4:low angle.

5:dolliyng
6:tilt
7:zoom

8:pan
sikiliza ngoma tam wa banana zoro ni wimbo wenye maana kubwa hasa kwa wale wapendanao.........>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Wednesday, November 11, 2015

hi ni ngoma kale ya mo music.................................>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>