MAKALA.
NINI SULUHISHO LA TATIZO LA
MAJI NJOMBE?
Na
jimsoni myinga;
Maji ni kimiminika mhimu sana kwa
maisha ya kila siku kwa binadamu yeyote, maji yana umuhimu mkubwa sana katika
kuletea maendeleo ya eneo lolote lile, maji pia ni muhimu sana katika maisha ya
viumbe hai kama mimea,wadudu na wanyama.
Vipo vyanzo vingi sana vya
maji kuna mabwawa,mito na maziwa.Kwa kuanza tatizo la maji njombe limekuwa
kubwa sana kadri siku zinavyozidi kwenda, tatizo hilo la maji mkoa wa njombe
limekuwa kubwa kiasi cha kufikia kukithiri sana baina ya wananchi na wakazi wa
mkoa huu.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wakazi wa mkoani njombe wakazi wa kata ya njombe mjini na kata ya
ramadhani wamesena tatizo hilo la maji limekuwa kero sana kwao, wakiendelea
kuelezea adha hiyo ya maji inyo wa kabili wananchi hao na wakazi wa mkoa huo wa
njombe wamesema wanaomba mamlaka zote zinazo husika na kutatua tatizo hilo
kulishughulikia tatizo hilo kwa haraka kadri inavyo wezekana.
Wakazi hao wa kata hizo za
njombe mjini na ramadhani waliendelea kwakusema kuwa wamechoshwa na maneno na
ahadi za wanasiasa na viongozi wengi waoishia kuwa ahidi tu kuwa watamaliza
tatizo hilo haraka iwezekanvyo na hatimye hawa tekelezi ahadi hizo kwa wakati.Wakiendelea kulalama
kwa hisia wananchi hao mithiri ya mbogo walio jeruhiwa walisema tatizo hilo la
maji limepelekea matatizo mengi sana kama vile watoto kuchelewa shule, hapa
inasababishwa na foleni kubwa wanayo kumbana nayo pale wanapo jihimu kwajili ya
kwenda kuyasaka maji hayo katika mabomba ambayo miundombinu yake imechoka sana
nakuto mudu uhitaji wa wananchi wa maeneo hayo “yaani ni kama mgonjwa
anakaribia kupoteza uhai wake”.
Nilifurahishwa sana na
kauli mbalimbali walizokuwa wakizitoa wakiziirisha dhahiri wamechoshwa na hali
hiyo ya maisha wanayoishi na nukuu “wananchi tunapata shida mithiri ya
wakimbizi katika nchi yetu wenyewe, tunataabika sana na wengine ndoa zetu
zimekuwa hatarini kwasababui tu waumezetu wanakosa maji ya kuoga”.
Wakiendelea kutoa kero hizo
wanasema pia maji ni muhimu sana katika kuimarisha afya zao, maji yanavyo
kosekana wanashindwa kufanya usafi wa vyombo vyao na maeneo muhimu kama vyooni
na mabafuni hali hiyo inapelekea kulipuka kwa magonjwa kama kipindupindu na
homa za matumbo.
Ndipo nikalazimika kubisha
hodi katika ofisi za mamlaka husika inayohusika na “maji safi na maji taka” mkoani
hapa.Nikizungumza na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka
mkoani njombe amesema “Kama mamlaka tuna tambua uwepo wa tatizo la maji mkoani
hapa na hali hii imesababishwa na ongezeko kubwa la watu mkoani hapa,Nasababu
nyingne ikiwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya maji mkoani hapa”.
Akizungumza mkurugenzi mtendaji huyo wa maji
taka na maji safi amesema tatizo hili
lipo mbioni kutatuliwa kwakuwa kuna mradi mkubwa wa maji ambao mda sio mrefu
utakuwa tayari na wananchi watapata maji yakutosha masaa24 na kusahau adha hiyo
iliyo wakumba kwa mda mrefu.
Usikose kupata mwendelezo
wa nakala hii wiki lijalo......................
No comments:
Post a Comment